Wapiganaji wa Hamas wauawa na Israel

Imebadilishwa: 24 Oktoba, 2012 - Saa 08:17 GMT


Wapiganaji wawili wa kundi la Hamas wameuwa na wengine kujeruhiwa huko Gaza na kombora la andani lililorushwa na wanajeshi wa Israel.

Wanajeshi hao wanasema kuwa kombora hilo liliwapata wapiganaji hao wakipanga kuishambulia Israel kwa roketi.

Roketi kadha zilielekezwa Israel mapema Jumanne na afisa mmoja wa Israel alijeruhiwa kutokana na mlipuko mpakani.

Shambulio hilo lilitokea saa chache tu baada ya kiongozi wa Qatar kufanya ziara ya kwanza ya kiongozi wa nchi tangu Hamas ichukue uongozi miaka mitano iliyopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.