Mkalimani apewa hifadhi Uingereza

Imebadilishwa: 24 Oktoba, 2012 - Saa 08:11 GMT


Uingereza imempa hifadhi mkalimani kutoka Afghanstan ambaye alikuwa amepokea vitisho vya kuuwawa kutoka kwa kundi la Taleban kwa kushirikiana na Jeshi la Uingereza.

Mohammad ambaye hawezi kujitambulisha kikamilifu ili kuiokoa familia yake nchini Afghanistan, alijeruhiwa katika shambulizi la bomu mwaka 2007.

Alikuwa ameonywa kuwa maisha yake yatakuwa hatarini endapo angerejea Afghanistan.

Awali serikali ya Uingereza ilikuwa imekataa kukubali ombi lake lakini ikabadilisha msimamo baada ya kupata habari kamili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.