Ukataji haramu miti DRC wakithiri

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 14:24 GMT

Ripoti kuhusu ,ukataji haramu wa miti katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeelezea kuwa maafisa wa nchi hiyo pamoja na wakuu wa kampuni za kigeni,wanavunja sheria za nchi hiyo ambazo zinapaswa kuzuia kukatwa kwa miti kwa kiwango kikubwa.

Uchunguzi uliofanywa na mashirika mawili ya wanaharakati wa mazingira, unatuhumu wafanyabiashara wa mbao kwa kuhujumu sheria za nchi hiyo zinazopiga marufuku kutolewa vibali vya kukata miti.

Wanaharakati hao wanasema kuwa DRC ndiyo nchi ya pili yenye misitu mingi duniani na ina wakataji wa miti ambayo inakabiliwa na tisho la kuangamia na ambayo ina soko kubwa nchini China.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.