Syria kusitisha vita wakati wa Eid

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 13:20 GMT

Kundi la wachunguzi wa haki za kibinadam la umoja wa mataifa limewasilisha rasmi ombi la kukutana na Rais wa Syria Basher al Assad kwa mara ya kwanza tangu Majeshi yake yaanze kupigana na wanamgambo wanaotaka kuipindua serikali yake .

Kundi hili linalongozwa na aliyekuwa kiongozi wa wapelelezi wa umoja huo, Carl del Ponte limesema lina jukumu la kushughulikia makosa mengi tu ya jinai ambayo yamefanyika .

Wakati huohuo serikali ya syria inatarajiwa kutangaza wakati wowote iwapo imekubali kusitisha mapigano dhidi ya waasi kwa kipindi cha siku nne ili kuwaruhusu wasyria kuadhimisha sikukuu ya Eid ul Adha kuanzia ijumaa .

Habari za maafikiano ya kusitisha mapigano zilitangazwa jana na mpatanashi wa umoja wa mataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi.

Lakini jeshi la taifa hilo likataka kutangazwa rasmi kwa amri hiyo ya kusitishwa mapigano ikidai muda zaidi kutathmini athari kwa pande zote mbili katika mzozo huu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.