Wito kuhusu bajeti za Ulaya waungwa mkono

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 08:16 GMT

Mkuu wa benki kuu ya Ulaya,Mario Draghi, amesema ataunga mkono pendekezo la kuupa usemi mkubwa Umoja wa Ulaya kuhusu bajeti za nchi wanachama wa Umoja huo.

Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani der Spiegel, Draghi amesema hatua kama hiyo ni muhimuili watu kuweza kuwa na imani katika sarafu ya euro inayotumika Ulaya.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara anasema matamshi ya Draghi huenda yakakaribishwa nchini Ujerumani, nchi ambayo ambayo imekuwa ikidai kwamba Umoja wa Ulaya ni lazima uwe na uwezo wa kuzuia mipango ya matumizi ya kitaifa. Na kwamba iwapo mataifa yatavunja sheria zilizoidhinishwa kudhibiti nakisi za bajeti za nchi tofauti.

Hata hivyo, anasema hatua kama hiyo itahitaji mabadiliko katika mkataba wa makubaliano ya Ulaya, katika wakati ambapo nchi kadhaa zinakataa kutoa uwezo zaidi kwa Umoja huo wa Ulaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.