Kesi ya kufichua wanaokwepa kodi Ugiriki

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 08:07 GMT

Mhariri wa jarida moja nchni Ugiriki, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo akikabiliwa na mashtaka ya kukiuka faragha.

Hii ni baada ya yeye kuchapisha orodha ya majina elfu mbili ya matajiri nchini humo wanaoshukiwa kusafirisha na kuzificha fedha katika benki za Uswizi ili kukwepa kulipa kodi.

Katika kanda ya video mhariri huyo,Kostas Vaxenavis amelalamika kuwa wanasiasa wa Ugiriki wako tayari kuidhinisha mpango wa kupunguza matumizi ya pesa za umma lakini hawajashughulika katika kuwachunguza washukiwa wa kukwepa kulipa kodi.

Orodha ilipelekwa kwanza bungeni miaka miwili iliyopita na mkuu wa sasa wa shirika la fedha ulimwenguni, IMF, Christine Lagarde, ambaye alikuwa waziri wa fedha nchini Ufaransa wakati huo.

Haijabainika iwapo orodha hiyo iliyochapishwa na Vaxenavis ni sawa na ile iliyowasilishwa bungeni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.