Demokrasia yadhihirika kwenye uchaguzi Ukrain

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 07:56 GMT

Chama tawala nchini Ukraine, Party of Regions, kinachoongozwa na Rais Viktor Yanukovich, kinadai kushinda katika uchaguzi wa ubunge uliofanyika jana.

Matokeo ya mapema yalionyesha kuwa chama hicho kinaongoza kwa kura nyingi, jambo lililosababisha viongozi wake kusema kuwa matokeo yanaonyesha kuwa wananchi wana imani na kiongozi wao.

Hata hivyo kutokana na mfumo tata wa uchaguzi nchini humo,matokeo rasmi huenda yakachukua muda kutolewa.

Awali kura za mwisho zilionyesha chama cha upinzani Fatherland, cha waziri mkuu wa zamani aliyefungwa gerezani, Yulia Tymoshenko, kiilijinyakulia chini ya asilimia 25 ya kura hizo.

Miongoni mwa vyama vinavyotarajiwa kuingia bungeni kwa mara ya kwanza ni pamoja na chama cha bingwa wa masumbwi Vitaly Klitschko, Punch, kinachopinga rushwa na kile cha mrengo wa kulia Nationalist Freedom Party.

Marekani na Umoja wa Ulaya zinaona uchaguzi huo kama kiashiria cha hadhi ya demokrasia nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.