Wafungwa kwa kutunga nyimbo Vietnam

Imebadilishwa: 30 Oktoba, 2012 - Saa 10:22 GMT

Mahakama nchini Vietnam imewafunga jela wasanii wawili wa muziki kwa kusambaza propaganda dhidi ya serikali.

Nyimbo zao zilikosoa China na kueleza malalamiko kuhusu ambavyo Vietnam ilishughulikia uhusiano kati yake na China.

Mmoja wa wasanii hao,Tran Vu Anh Binh, alihukumiwa miaka kumi gerezani, na mwenzake Viet Khang, kupokea kifungo cha miaka minne.

Shirika la Amnesty International limetaja hukumu hizo kama mzaha mkubwa.

Mwaka jana kulikuwa na maandamano kadhaa dhidi ya China nchini Vietnam,hali iliyochochewa na mzozo wa mpaka kuhusu visiwa vya Kusini mwa China.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.