Mauaji ya Imamu urusi yazua taharuki

Imebadilishwa: 30 Oktoba, 2012 - Saa 15:15 GMT

Watu waliojihami kwa bunduki katika eneo la North Caucasus nchini Urusi walimpiga risasi na kumuua mhubiri wa Kiislamu alipokuwa akielekea msikitini kwa sala ya alfajiri.

Imam Kalimullah Ibragimov aliuawa pamoja na babake na nduguye katika mji wa Derbent huko Dagestan. Inaaminika kuwa huyo ni imamu wa nne kuuawa katika eneo hilo mwaka huu.

Dagestan imeshuhudia ongezeko la wapiganaji na waislamu wenye siasa kali wanaoshinikiza kuundwa kwa taifa la kiislamu licha ya upinzani mkali kutoka kwa serikali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.