Mateka hawakulipiwa kikombozi Nigeria

Imebadilishwa: 1 Novemba, 2012 - Saa 12:02 GMT

Kampuni moja ya mafuta nchini Ufaransa, inasema kuwa wafanyakazi wake waliokuwa wametekwa nyara kutoka kwa meli pwani ya Nigeria, wiki mbili zilizopita wameachiliwa.

Kampuni hiyo Bourbon, imesema kuwa wafanyakazi hao sita rais wa Urusi na raia mmoja kutoka Estonian walikuwa bukheri wa afya walipoachiliwa.

Mamia ya watu wametekwa nyara katika eneo la Niger Delta, lenye utajiri wa mafuta ingawa duru zinasema kuwa tangu msamaha kutolewa kwa maharamia mwaka 2009 visa vya uharamia vimepungua.

Mateka wengi huachiliwa baada ya kulipiwa kikombozi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.