Kesi dhidi ya mhariri kuanza leo Ugiriki

Imebadilishwa: 1 Novemba, 2012 - Saa 09:18 GMT

Kesi dhidi ya mhariri wa jarida moja nchini Ugiriki aliyechapisha orodha ya watu wanaoshukiwa kukwepa kulipa ushuru inatizamiwa kuanza rasmi baadaye hii leo mjini Athen.

Mhariri huyo, Kostas Vaxevanis, anatuhumiwa kuvunja haki ya kutoingiliwa kwa kuchapisha orodha yenye majina ya raia elfu mbili wa Ugiriki walio na akaunti za benki nchini Uswizi.

Stakabadhi hizo awali ziliwasilishwa kwa serikali mnamo mwaka elfu mbili na kumi lakini uchunguzi haukufanywa.

Akizungumza na BBC, Vaxevanis alisema kuwa wanasiasa waliokosa kufanya uchunguzi wanafaa kushtakiwa. Alisema hawakuchukua hatua kwa kuwa baadhi ya wale waliotajwa walikuwa na uhusiano wa karibu na mawaziri.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.