Bloomberg amuunga mkono Obama

Imebadilishwa: 2 Novemba, 2012 - Saa 10:08 GMT
Michael Bloomberg

Michael Bloomberg

Mada ya mabadiliko ya anga imehusishwa katika kampeni za urais nchini Marekani haswa baada ya meya wa jiji la Newyork kusema mada hiyo ndio iliyomfanya kumuunga mkono Barrack obama.

Meya wa mji wa New York, Michael Bloomberg, amesema kuwa anamuunga mkono Rais Barrack Obama katika uchaguzi wa Urais kufuatia kimbunga kikali kilichokumba eneo la pwani ya kaskazini mashariki mwa Marekani.

Bloomberg, ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Republican, na asiyeegemea mrengo wowote kisiasa hivi sasa, amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Obama na mpinzani wake Mitt Romney.

Lakini sasa amesema kuwa Obama ndiye mombeaji bora zaidi anaeweza kutatua vyema swala la mabadiliko ya hali anga duniani ambayo anasema imechangia pakubwa kutoka kwa kimbunga Sandy, kilichosababisha maafa na hasara ya mamilioni ya madola nchini Marekani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.