Wanajeshi wa Marekani Matatani Japan

Imebadilishwa: 2 Novemba, 2012 - Saa 10:39 GMT
Wanajeshi wa Marekani

Wanajeshi wa Marekani

Maafisa wa serikali ya Japan, wamesema kuwa wamewasilisha rasmi malalamiko yao, kwa balozi wa Marekani, Mjini Tokyo, baada ya mwanajeshi mmoja wa Marekani kutuhumiwa kumjeruhi kijana mmoja raia wa nchi hiyo.

Ripoti zinasema, mwanajeshi huyo aliiingia katika chumba kimoja katika kisiwa cha Okinawa, ambako alimpiga mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 13.

Mvulana huyo alianguka kutoka dirishani na alikimbizwa hospitalini.

Uhalifu unaohusishwa na wanajeshi wa Marekani, katika kisiwa hicho cha Okinawa, umekuwa chanzo cha mzozo wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Wanajeshi wote wa Marekani nchini Japan sasa wamepigwa marufu, ya kutembea nyakati za usiku, kufuatia tuhuma za ubakaji katika kisiwa hicho wiki mbili zilizopi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.