Mhariri aachiliwa huru Ugiriki

Imebadilishwa: 2 Novemba, 2012 - Saa 10:20 GMT

Mahakama moja nchini Ugirirki imemuachilia huru, mhariri wa jarida moja , anayetuhumiwa kuvunja sheria ya haki ya kutoingiliwa baada ya kuchapisha orodha ya watu wanaoshukiwa kukwepa kulipa ushuru.

Kostas Vaxe-vanis, alikuwa ametoa wazi majina ya raia elfu mbili wa Ugiriki, walio na akaunti katika benki za Uswizi, ikiwa ni pamoja na waziri mmoja wa zamani.

Wakili wake walisema kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote, na kuongezea kuwa hakukuwa na uvunjaji sheria yeyote.

Vaxevanis alisema wale waliofaa kushtakiwa ni wanasiasa walioficha ukweli kuhusu uwezekano wa watu kuepuka kulipa ushuru.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.