Upinzani wagawanyika Syria

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 09:37 GMT

Makundi ya waasi wanaopinga utawala wa Rais Assad nchini Syria yametofautiana vikali na kutishia kuvunja mkutano wao unaonuiwa kuleta muungano.

Makundi hayo yanakutana mjini Doha Qatar kutafuta namna ya kuunda serikali mbadala wakiwa nje ya nchi.

Hata hivyo kiongozi mmoja mkuu wa upinzani amejitokeza na kutangaza kuwa yeye ndiye aliyepata uungwaji mkono zaidi na mataifa ya nje, jambo lililopingwa vikali na waasi wa Syrian National Congress.

Waasi hao wameonya dhidi ya kuruhusu muingilio wa mataifa ya Magharibi katika mageuzi hayo.

Huku hayo yakijiri msemaji wa upande mmoja wa upinzani wa syria , Syrian National Council amesema kuwa madai ya kuwepo kwa mgawanyiko si ya ukweli na kuwa majadiliano yanaendelea kama ilivyopangwa jijini Qatar na kuwa majadiliano hayo hayatoathiri umuhimu wa baraza la kitaifa ambalo uanachama wake umekuwa ukishtumiwa kwa kuhusisha wasomi pekee na watu walio nje ya syria

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.