Walinzi wa mpakani wauawa Saudia

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 14:53 GMT

Wizara ya mambo ya ndani nchini Saudi Arabia inasema kuwa walinzi wawili wa mpakani wamepigwa risasi na kuuwawa katika uvamizi uliofanyika karibu na mpaka ulio Kusini na Yemen.

Wizara hiyo inasema kuwa inashuku wanamgambo wa kundi la Al Qaeda ndiyo waliohusika na shambulio hilo.

Imesema wanamgambo hao waliachiliwa hivi karibuni kutoka gerezani na walikuwa wanajaribu kuvuka na kuingia nchini Yemen.

Wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu walio na uhusiano na kundi hilo la Al Qaida, wengine kutoka Saudia wamekuwa wakijaribu kuyadhibiti maeneo yaliyo kusini mwa Yemen tangu mwaka jana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.