Taarifa za kifo cha Heywood Marekani

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 11:47 GMT

Gazeti moja nchini Marekani limechapisha madai mapya kuwa Neil Heywood ambaye ni mfanyabiashara wa Uingereza aliyeuawa Uchina mwaka jana alikuwa na uhusiano na mashirika ya kijasusi nchini Uingereza.

Gazeti la Wall street linasema marafiki wa Heywood wanasema amekuwa akitoa taarifa kwa M16 kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kufariki, licha ya kwamba hakuajiriwa na shirika hilo.

Neil Heywood alikuwa na ushirikiano wa karibu na mwanasiasa mmoja wa China mashuhuri Bo Xilai ambaye mkewe alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano gerezani kwa kumuua Heywood kwa sumu.

Waandishi wanaeleza kuwa iwapo hili ni kweli linazusha maswali mapya kuhusu kwanini serikali ya Uingereza haikutaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu kifo chake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.