Mwanaharakati matatani China

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 12:57 GMT

Mumewe mwanaharakati mmoja anayepinga sera ya wazazi kuzaa mtoto mmoja anasema kuwa mwanaharakati huyo amewekwa katika kambi ya kazi ngumu kwa miezi minane kwa mashtaka ya kutatiza utulivu wa jamii.

Mao Hengfeng ambaye ana mabinti watatu amezuiliwa mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni kwa kuikashifu serikali.

Hatua ya mwisho dhidi yake imechukuliwa wakati China imeshinikiza usalama huku mkutano wa chama tawala cha kikomunisti nchini ukiwadia siku ya Alhamisi.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International linasema zaidi ya raia mia moja wamezuiliwa au wamewekewa vikwazo.

Serikali ya Beijing imepiga marufuku vibofu, njiwa, na mifano ya ndege wanaotumiwa kusambaza vijikaratasi vya ujumbe wenye nia ya kushinikiza kupingwa agizo la serikali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.