Shambulizi la bomu Pakistan

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 15:23 GMT

Maafisa wa serikali kaskazini magharibi mwa Pakistan wanasema kuwa mlipuaji wa kujitoa mhanga, amewauawa afisa mmoja mwandamizi wa polisi na watu wengine wanne katika mji wa Peshawar.

Zaidi ya watu wengine thehini wanasemekana kujeruhiwa kwenye mlipuko huo, ambao ulitokea katika eneo lenye idadi kubwa ya watu.

Msemaji wa kundi la taleban nchini Pakistan amesema kundi hilo lilitekeleza shambulio hilo.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa katika miezi ya hivi karibuni, wapiganaji wa Taleban wamekuwa wakilenga maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la polisi ambao wanahusika na kuwakamata na kuwachunguza wapiganaji hao waasi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.