Uingereza kusitisha msaada kwa India

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 12:20 GMT

Uingereza inatarajiwa kusimamisha msaada wa kimaendeleo kwa India katika kile ambacho serikai ya Uingereza inasema ni kutambua mageuzi yaliofanikiwa katika kuwa sehemu muhimu ya uchumi duniani.

Kwa miaka mingi sasa wapinzani wa msaada wa maendeleo wameeleza kushangazwa kwa nchi ndogo kama Uingereza kuipa msaada nchi kubwa na inayostawi India.

Na hasa, kando na kuwa India ina nafasi ya miradi, na ina uchumi unaokuwa haraka, lakini pia, ina idadi ya watu sawa au pengine wengi zaidi walio maskini kuliko bara zima la Afrika.

Lakini angalau kutokana na mtizamo wa nchi ya Uingereza, mjadala huo sasa umekwisha, kwa kuwa wizara ya maendeleo ya kimataifa, kupitia waziri wa misaada wa Uingereza, Justine Greening, imetangaza kuwa msaada wote wa Uingereza kwa India utasitishwa kufikia mwaka 2015.

Hatua hiyo inatarajiwa kusaidia kuokoa dola milioni mia mbili na hamsini, kiwango kidogo katika bajeti nzima ya misaada ya nchi za nje ambayo kwa jumla ina thamani ya dola bilioni kumi.

Lakini kusitishwa kwa msaada huo, kutadhihirisha kuwa serikali inafahamu, kwamba katika hali mbaya iliopo ya uchumi, bajeti hiyo ya msaada inapaswa kutizamwa kwa makini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.