Mahakama kutoa hukumu kuhusu Abu Qatada

Imebadilishwa: 12 Novemba, 2012 - Saa 07:49 GMT

Mahakimu wa Tume Mahsusi ya Kukata Rufaa za Uhamisho mjini London wanategemewa kutoa hukumu leo kuhusu iwapo mhubiri wa Kiisilamu mwenye maoni makali, Abu Qatada, atahamishwa hadi Jordan ambapo anatuhumiwa kupanga mashambulio ya mabomu.

Mapema mwaka huu, Mahakama ya Ulaya Inayoshughulikia Haki za Binadamu ilipinga kuhamishwa kwake kwa madai kwamba ushahidi dhidi yake uliopatikana baada ya yeye kuteswa, ungetumika dhidi yake.

Serikali ya Uingereza imesema kwamba imepata hakikisho toka Jordan kwamba kesi yake itafanywa katika mazingira ya haki, lakini wakili wa Abu Qatada wanapinga hayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.