Uchunguzi dhidi ya asasi Australia

Imebadilishwa: 12 Novemba, 2012 - Saa 08:41 GMT

Waziri Mkuu wa Australia Julia Gillard ametangaza kuundwa kwa tume ya kitaifa itakayochunguza vile ripoti za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto zilishughulikiwa na asasi fulani.

Hii ni baada ya afisa wa kiwango cha juu wa polisi kudai kwamba Kanisa Katoliki huko New South Wales liliharibu ushahidi na kunyamazisha chunguzi kuhusu tetesi dhidi ya mapadri fulani walioshukiwa waliwadhulumu watoto kijinisa.

Bi Gillard alisema kwamba tume hiyo itachunguza taasisi za kidini, za kiserikali zinazotoa huduma za matunzo, NGO, polisi, pamoja na kutafuta maoni kutoka kwa mashirika yanayowashughulikia watoto.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.