Kesi dhidi ya mshirika wa Gadaffi kuanza

Imebadilishwa: 12 Novemba, 2012 - Saa 07:37 GMT

Kesi dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya hayati Muammar Gadaffi, Bwana Al-Baghdadi al-Mahmudi, inatarajiwa kuanza baadaye leo mjini Tripoli.

Al-Baghdadi al-Mahmudi alitorokea nchi jirani ya Tunisia Septemba mwaka jana, punde tu baada ya waasi kuuteka mji mkuu wa Libya na kukomesha zaidi ya miongo minne ya utawala wa Gadaffi.

Mshirika sugu wa Gadaffi, Al-Baghdadi al-Mahmudi alirudishwa Libya mwezi Juni mwaka huu, hata baada ya onyo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu kwamba kulikuwa na uwezekano angeteswa au kupewa hukumu ya kifo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.