Msaidizi wa aliyekuwa rais mashakani Brazil

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 09:53 GMT

Msaidizi mmoja mkuu wa aliyekuwa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amefungwa miaka kumi na miezi kumi gerezani kwa ufisadi.

Jose Dirceu ambaye alikuwa mkuu wa utumishi wa rais Lula kuanzi mwaka wa 2003 hadi 2005, alipatikana na hatia ya kuanzisha mpango haramu uliotumia fedha za umma kulipa vyama tofauti ili kupata ushawishi wa kisiasa.

Alikuwa miongoni mwa wakuu wa chama cha wafanyikazi, waliohukumiwa mwezi uliopita kwa kuhusika na sakata hiyo. Rais huyo wa zamani hata hivyo hakuhusishwa na kashfa hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.