Jumuiya kiarabu yapongeza upinzani Syria

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 09:45 GMT

Jumuiya ya nchi za kiarabu imesifu hatua ya kubuniwa kwa muungano wa upinzani nchini Syria, na kutaka makundi yote ya upinzani kujiunga nayo.

Pia umetaka muungano huo kutambuliwa kama mwakilishi halali wa maslahi ya raia wa Syria.

Hata hivyo mawaziri hao waliokuwa wakikutana mjini Cairo walikosa kufafanua iwapo wanautazama muungano huo kama sauti ya pekee ya raia wa Syria.

Mapema Jumatatu mataifa hayo sita ya baraza la ushirikiano la Ghuba, yalitangaza kuwa yanaunga mkono na kutambua muungano huo.

Waandishi wa habari wanasema umoja wa nchi za kiarabu umesita tuu kuunga mkono kikamilifu muungano huo, huku baadhi ya mataifa ya eneo hilo, yakikosa kauli ya pamoja kuhusu utawala wa Rais Bashar AL Assad.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.