Obama azungumzia sakata ya Petraeus

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 12:34 GMT

Rais Obama anasema hana ushahidi wowote kuwa usalama wa kitaifa wa Marekani uliwekwa katika hatari na sakata iliyopelekea kujiuzulu kwa Mkuu wa Idara ya ujasusi David Petraeus.

Obama amesema hatatoa uamuzi hadi uchunguzi wa sakata hiyo utakapokamilika.

Wakati huo huo, kamanda mkuu wa Marekani nchini Afghanistan Jenerali John Allen, amesema atashirikiana kikamilifu na uchunguzi wa mawasiliano na mwanamke wa pili anayehusika katika sakata hiyo, Jill Kelley.

Ilikuwa ni malalamishi yake ya kunyanyaswa na Paula broadwell, yaliyopelekea uchunguzi uliomlazimu Petreaus kukiri kuwepo kwa uhusiano huo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.