Mwanajeshi ayongwa Pakistan

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 12:39 GMT

Pakistan imenyonga mwanajeshi aliyeshtakiwa kwa mauaji ya afisa wake mkuu baada ya rufaa ya mwanajeshi huyo kuomba msamaha kutupiliwa mbali.

Hii ni hukumu ya kwanza ya kunyongwa nchini humo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Pakistan imesitisha hukumu za kifo tangu rais Asi Ali Zardari, alipochukua hatamu za uongozi mwa 2008.

Hata hivyo, makundi ya kutetea haki za Binadamu yamesema nchi hiyo ina idadi kubwa zaidi ya wafungwa waliohukumiwa kifo inayokisiwa kufikia elfu nane.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.