CIA kumchunguza Patraeus

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 10:27 GMT
David Petraeus

David Petraeus

Shirika la upelelezi la CIA nchini Marekani linasema limeanzisha uchunguzi kufuatia kujiuzulu kwa mkurugenzi wake mkuu Jenerali David Petraeus, wiki iliyopita, kutokana na kashfa ya kimapenzi.

David Petraeus alijiuzulu baada ya kukiri kuwa na uhusianao wa kimapenzi na mwandishi wa kitabu chake Paula Broadwell.

Siku ya Jumatatu, maafisa wa FBI waliondoa komputya kutoka nyumbani kwake wakisema alikuwa na stakabadhi za siri za serikali.

Lakini Jenerali anasema hajawahi kuumpa Broadwell stakabadhi kama hizo.

Baadaye Leo Ijumaa, David Petraeus anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya Bunge kuhusu ujasusi kutoa taarifa kuhusu kilichotokea wakati ubalozi wa marekani katika mji wa Benghazi nchini Libya, uliposhambuliwa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.