Mashambulio zaidi Gaza

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 10:23 GMT
Mashambulio ya Gaza

Mashambulio ya Gaza

Milipuko imeendelea usiku kucha katika eneo la Gaza, huku Israel ikiimarisha mashambulio yake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Palestina, Hamas.

Mwandishi wa BBC mjini Gaza, anaripoti kusikia milipuko mikubwa leo alfajiri.

Mkaazi mmoja mjini Gaza ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Raji Sourani, anasema umekuwa usiku mgumu mno kwa raia wengi kutokana na mashambulio hayo.

Israel inasema imelenga zaidi ya shabaha mia tatu thelathini usiku wa kuamkia leo.

Pia imesema wanamgambo hao wa Palestina wamefyatua zaidi ya makombora kumi nchini Israel.

Serikali ya Israeli imetoa idhini kwa jeshi nchini humo kuwaita wanajeshi elfu thelathini wa ziada, huku kukiwepo uvumi kuwa huenda shambulio la ardhini dhidi ya Gaza linapangwa.

Takriban wapalestina kumi na wanane na waisraeli watatu wameuwawa tangu Israeli kumuua kiongozi wa kundi la Hamas Jumatano.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.