Obama kushauriana na wabunge wa Congress

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 15:25 GMT

Rais Barack Obama, anatarajiwa kushauriana na viongozi wa bunge la Congress, kwa mara ya kwanza hii leo, tangu alipochaguliwa kwa awamu nyingine, kujaribu kuzuia kutokea kwa mzozo wa bajeti.

Ikiwa rais Obama na viongozi hao hawataafikiana lolote kabla ya mwisho wa mwaka huu, viwango vya ushuru vitaongezeka na serikali italazimika kupunguza matumizi yake, kwa mujibu wa sheria mpya itakayoanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.

Rais Obama, tayari amesisitiza kuwa raia wa nchi hiyo wenye mapato ya juu, washurutishwe kulipa ushuru zaidi lakini chama cha republican, ambacho kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge hilo,kimepinga vikali pendekezo hilo la rais Obama.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.