Gotovina aachilliwa huru na ICC

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 12:55 GMT
Ante Gotovina na Mladen Markac

Ante Gotovina na Mladen Markac

Mahakama ya rufaa ya Hague imemwondolea Generali wa zamani wa Crotia, Ante Gotovina hatia ya kushiriki katika mauaji wakati wa mzozo wa uliyokuwa nchi ya Yugosolavia miaka ya tisini.

Bwana Gotovina, alifungwa kwa miaka ishirini na minne baada ya mahakama kumhusisha na mauji ya mamia ya raia wa serbia.

Hata hivyo mshukiwa huyo alikataa rufaa na kusema kuwa hakudhamiria kuwauwa raia.

Kadhalika mahakama ilibatilisha uamuzi wa kumtia hatiani kamanda wa zamani wa polisi wa Croatia, Mladen Markac na kuagiza wote wawili waachiliwe huru.

Uamuzi huo uliokuwa umesubiriwa kwa hamu kubwa umempa umaarufu mkubwa bwana Gotovin

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.