Bal Thackeray Azikwa India

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 13:31 GMT

Shughuli zimesimama katika jiji la Mumbai, India, wakati maelfu ya waombolezaji wamejaa mabarabarani, kwa ajili ya mazishi ya mwanasiasa mmoja wa India, maarufu na mtatanishi, Bal Thackeray.

Serikali ya nchi hiyo imetanga leo kuwa siku ya maombolezi ya kitaifa wakakti mazisha ya kitaifa mwanasiasa huyo maarufu yakifanyika.

Maiti yake ilifunikwa bendera ya India na kupambwa kwa maua ilipitishwa katikati ya umati mkubwa wa watu.

Bal Thackeray alikuwa mmoja kati ya wanasiasa walioleta mgawanyiko mkubwa katika siasa za India.

Aliheshimiwa sana na wafuasi wake huku akiogopwa na makabila madogo na kupingwa vikali na wengi wengine.

Alishutumiwa kuwa akichochea ghasia dhidi ya Waislamu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.