Wanajeshi Nigeria wakanusha madai ya mauaji

Imebadilishwa: 19 Novemba, 2012 - Saa 07:14 GMT

Shirika la habari la Reuters limetoa kanda ya video inayosemekana inaoonyesha wanajeshi wa Nigeria wakimpiga risasi na kumuua mtu waliyekuwa wamemkamata.

Kanda hiyo, ambayo haijathibitishwa wa wathibithsaji huru, inaonyesha mwanamume mmoja akiomba asiuwawe, kabla ya kupigwa risasi kati ya maiti nyingine. Kanda hiyo aidha inaonyesha wanajeshi hao wakiipiga miili hiyo risasi pia.

Hata hivyo Jeshi la Nigeria limetupilia mbali kanda hiyo likisema kwamba ni uwongo mtupu, na kwamba wanajeshi wa jeshi hilo hawawezi kutenda vitendo kama hivyo.

Awali, Jeshi la Nigeria limekuwa likilaumiwa kwa kuwaua watu kiholela katika juhudi zake dhidi ya kikundi cha Kiisilamu chenye siasa kali cha Boko Haram.

Reuters inasema ilipewa kanda hiyo na mwanajeshi aliyesema kwamba alishuhudia mauaji hayo wiki mbili zilizopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.