Benki ya Dunia yaonya kuhusu hali ya hewa

Imebadilishwa: 19 Novemba, 2012 - Saa 08:34 GMT

Benki ya Dunia imeonya kwamba vipimo vya joto duniani vinaweza kuongezeka kwa alama 4 Celsius ifikapo mwisho wa karne hii, iwapo juhudi zaidi za kutunza mazingira ili kupunguza makali ya kubadilika kwa hali ya hewa hazitachukuliwa.

Ripoti ya benki hiyo imesema kuwa dunia nzima inakumbwa na kupanda kwa viwango vya bahari, ukosefu wa chakula, hali mbaya ya hewa – huku nchi maskini zikiathirika zaidi

Inasema kuwa kuna uwezekano wa kupanda kwa kiwango cha joto kwa alama 3 Celsius, hata kama nchi zote zitafikia malengo yao ya kupunguza athari zijulikanazo kama “greenhouse”.

Raisi wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim, alisema umaskini hautaangamizwa iwapo dunia nzima haitazingatia mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.