Sarkozy afika mahakamani

Imebadilishwa: 21 Novemba, 2012 - Saa 15:13 GMT

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy hii leo amefika mbele ya jaji mjini Bordeaux kujibu tuhuma kwamba alikubali msaada usiokubalika kisheria.

Sarkozy anatuhumiwa kupokea melfu ya madola kwa niaba ya chama chake kutoka kwa mwanamke tajiri wa Ufaransa ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya vipodozi ya Loreal Liliane Bettencourt, kwa ajili ya kudhamini kampeni zake mwaka 2007.

Bwana Sarkozy amejiondoa kwenye ulingo wa kisasa tangu aliposhindwa mwezi Mei , lakini kuna tetesi kuwa huenda akawania kugombea tena mwaka 2017.

Bwana Sarkozy alikanusha madai hayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.