Watoto wanyanyaswa Uingereza

Imebadilishwa: 21 Novemba, 2012 - Saa 18:51 GMT

Watoto Uingereza wanyanyaswa

Ripoti inayoangazia unyanyasaji wa watoto England pekee inaonyesha kuwa zaidi ya watoto elfu mbili na mia nne walinyanyaswa katika kipindi cha miezi kumi na nne-mwaka 2010 na 2011 na kuongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa.

Ripoti ya ofisi ya serikali inayoshughulikia watoto imesema unyanyasaji huo ni pamoja na kutekwa, biashara haramu ya usafirishaji wa watoto, kupigwa au kutishwa na katika baadhi ya matukio wamekuwa wakibakwa mara kwa mara na vijana kutoka maeneo jirani na wanapoishi.

Inasema magenge ndio yanayohusika zaidi na baadhi ya ukatili huo ambao mwingi unatokea bila kujulikana. Kitengo che elimu kimesema kitafuatlia matokeo ya utafiti huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.