Mshukiwa wa mashambulio akamatwa

Imebadilishwa: 23 Novemba, 2012 - Saa 10:36 GMT

Maafisa wa Israel wamemkamata mwanamume mmoja raia wa nchi hiyo, mwenye asili ya kiarabu anayedhaniwa kuhusika katika shambulizi la bomu katika basi moja huko Tela aviv Jumatano.

Watu ishirini na tisa walijeruhiwa katika tukio hilo ambalo lilifanyika saa chache tu kabla ya kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas yaliyochukuwa siku nane.

Shambulio hilo lilikuwa la kwanza kufaulu Tel Aviv kwa takriban miaka sita.

Kwa sasa watu wa Gaza na Kusini ya Israel wana utulivu ambao umetokana na kusitishwa mapigano ya wiki moja kutoa nafasi ya mazungumzo baina ya pande hizo mbili zinazozozana.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.