Waliokuwa wanajeshi Australia walalamika

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 06:06 GMT

Serikali ya Australia imewaomba msamaha wanaume na wanawake wote waliodhulumiwa walipokuwa wanahudumu katika majeshi ya ulinzi ya taifa hilo.

Zaidi ya watu 1,000 wamejitokeza katika miezi ya hivi karibuni na kutoa madai kuhusu dhuluma walizotendewa, zikiwemo ubakaji.

Baadhi ya visa hivyo vikitokea miaka mingi iliyopita, hata katika miaka ya 1950s.

Akizungumza bungeni, Waziri wa Ulinzi Stephen Smith alisema wengi wao waliathirika vibaya baada ya kutendewa dhuluma za kufedhehesha.

Jopo maalum limebuniwa ili kupokea malalamishi, pamoja na kutoa fidia kwa wale walioathiriwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.