Rais wa Misri kukutana na mahakimu

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 05:48 GMT

Rais wa Misri Mohammed Morsi ameanzisha juhudi za kuafikia maridhiano na wapinzani wake katika mzozo unaozidi kutokota kuhusiana na uamuzi wake wa kujilimbikizia madaraka mengine makubwa.

Bwana Morsi amesema uamuzi wake wa wiki iliyopita wa kujipatia madaraka ya kuitawala Misri bila kupingwa ni hatua ya muda tu.

Kwa ajili hiyo, Morsi anakusudia kukutana na mahakimu wa ngazi za juu katika juhudi za kupunguza makali ya mzozo huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.