Rais wa Mauritania arudi nyumbani

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 06:51 GMT

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdelaziz amerudi nyumbani kwa mara kwanza tangu ajeruhiwe na mwanajeshi mmoja mwezi uliopita.

Rais Abdelaziz alipigwa risasi mkononi na mwanajeshi huyo katika tukio ambalo serikali ilisema ilikuwa ni bahati mbaya.

Amekuwa Ufaransa kwa matibabu kwa majuma sita sasa.

Maelfu ya wananchi walikusanyika katika kiwanja cha ndege ili kumlaki raisi huyo aliporudi Nouakchott.

Wanahabari walisema kuwa afya ya kiongozi huyo, mwenye miaka 55, ilionekana nzuri, na kwamba aliwapungia mkono watu kutoka kwa gari lake ingawaje hakuwazungumzia.

Mwanajeshi huyo aliiambia runinga mwezi uliopita kwamba alililifyatulia risasi gari moja ambalo lilikuwa halieleweki pasipokujua kwamba rais alikuwemo mle ndani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.