Balozi alitoa taarifa za kupotosha

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 08:41 GMT

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amekiri kwamba alitoa habari zisizokuwa sahihi kufuatia shambulio lililotekelezwa dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani nchini Libya mwezi Septemba.

Shambulio hilo lilisababisha kifo cha balozi wa marekani nchini Libya Christopher Stevens.

Akizungumza mbele ya bunge la Senate nchini Marekani Bi. Susan Rice amesema alikosea kwa kusema kuwa shambulio hilo lililotokea katika mji wa Benghazi lilifuatia maandamano yaliyozuka ghafla na wala sio shambulio lililopangwa na magaidi

Lakini maseneta hawakukubaliana na maelezo yake na wakaapa kujaribu kupinga mpango wa Rais Obama kumteuwa Bi. Rice kama waziri wa mashauri ya nchi za kigeni kuchukuwa wadhfa wa Bi Hillary Clinton mwaka ujao.

Chama cha Democrat kina idadi kubwa ya wabunge katika Senate lakini kinahitaji msaada wa chama ch Republican ili kuidhinisha uteuzi wa Bi. Rice.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.