Wapinga jeshi kuwazuia wanawake Marekani

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 08:21 GMT

Chama cha kupigania haki za kiraia nchini Marekani kimewasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa jeshi la taifa hilo kuwapiga marufuku wanajeshi wa kike kufanya kazi katika maeneo ya vita.

Chama hicho ambacho kiliwasilisha kesi hiyo kwa niaba ya wanajeshi wanne wa kike kinasema sera hiyo inakiuka katiba.

Kundi hilo linasema licha ya hatua ya kulegeza sera hiyo katika miaka ya hivi karibuni, wanawake bado wananyimwa fursa ya kuhudumu katika nyadhfa zaidi ya mia mbili vitani katika jeshi la Marekani.

Msemaji katika afisi ya waziri wa ulinzi, Leon Panetta, amesema kuwa takriban nyadhfa elfu kumi na tano za kivita katika jeshi la Marekani zimetolewa kwa wanawake tangu achukue hatamu za uongozi katika wizara hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.