Urusi na Uturuki kukutana kuhusu Syria

Imebadilishwa: 3 Disemba, 2012 - Saa 08:54 GMT


Vita vinavyozidi vya ndani nchini Syria, vinatarajiwa kugubika mazungumzo mjini Istanbul katika masaa kadha yanayowadia kati ya rais wa Uturuki na wa Urusi.

Rais Vladimir Putin amekuwa akiunga mkono serikali ya Syria katika miezi ishirini iliyopita ya mapigano, huku waziri mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan, akiwa anawaunga mkono waasi wa Syria.

Mwandishi wa BBC mjini Istanbul anasema Putin huenda akazusha suala la ombi la Uturuki kwa jumuiya ya kujihami NATO la kutuma makombora katika mpaka wake na Syria.

Urusi imeonya dhidi ya hatua kama hiyo. Nchini Syria kwenyewe vikosi vya serikali vinaendelea kuzishambulia wilaya zinazodhibitiwa na wanamgambo mjini Damsacus kwa kutumia makombora na silaha nyengine nzito.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.