Wakimbzi wa Syria mashakani

Imebadilishwa: 4 Disemba, 2012 - Saa 09:12 GMT

Shirika la msaada, Save the Children, limeonya kuwa ukosefu wa msaada unaathiri jitihada za kimataifa kuwasaidia wakimbizi wa Syria wakati msimu wa baridi unawadia.

Linasema hakuna nguo nzito, blanketi na makaazi ya kutosha. Shirika hilo linasema theluji na baridi kali zitaifanya hali kuwa mbaya zaidi katika wiki zinazokuja.

Hazina maalum iliyoundwa kuwasaidia wakimbizi ina upungufu wa dola milioni mia mbili.

Hapo jana Umoja wa mataifa ulitangaza kuwa unaondoa wafanyakazi wake wasio hitajika nchini Syria kutokana na mzozo unaozidi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.