Marekani yasihi Israel kuhusu makaazi

Imebadilishwa: 4 Disemba, 2012 - Saa 09:08 GMT

Marekani imeiomba Israeli kufikiria upya kuhusu mpango wake wa kujenga maelfu ya nyumba katika ukingo wa magharibi na Jerusalem mashariki.

Msemaji wa Ikulu Marekani, Jay Carney, amesema kuwa hatua hiyo inakwamisha jitihada za kupatikana amani na Palestina.

Nchi kadhaa za Ulaya zikiwemo Ufaransa na Uingereza zimewaita mabalozi wao kulalamika kuhusu mipango hiyo.

Wakati huo huo Israeli imekataa shutuma za kimataifa, ikisema itaendelea na msimamo wake wenye faida muhimu.

Wapalestina wanasema mpango huo mpya uliopendekezwa wa ujenzi wa makaazi utaligawanya taifa ambalo huenda likawa la Palestina katika siku zijazo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.