400 wafariki kwenye kimbunga Phillipines

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 09:47 GMT

Takriban watu mia nne wamethibitishwa kufariki wiki hii katika kimbunga kikali katika maeno ya Kusini na kati mwa Ufilipino .

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni jamii za wafugaji katika bonde la Compostela, Mashariki mwa Mindanao, yaliyogubikwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Maiti za waathiriwa bado zinaondolewa kutoka kwa matope hayo ya maporomoko huku shuguli ya ujenzi ikianza.

Wahudumu wa misaada wanasema mojawapo ya shuguli za dharura, ni kutoa makaazi mbadala kwa mamia ya maelfu ya watu waliopoteza nyumba zao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.