Urusi kulipiza kisasi sheria ya Marekani

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 09:24 GMT

Urusi inasema italazimika kulipiza kisasi dhidi ya sheria mpya ya Marekani inayowawekea vikwazo maafisa wa Urusi wanaotuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Taarifa kutoka wizara ya nchi za kigeni mjini Moscow imetaja hatua hiyo kama la kushangaza.

Awali Bunge la Congress lilitoa idhini ya mwisho kwa sheria hiyo kama mojawapo ya hatua za kumaliza vikwazo vya vita baridi, vilivyozuia biashara kati ya Marekani na Urusi.

Iwapo itatiwa saini na Rais Obama, sheria hiyo itawazuia maafisa wa Urusi waliotuhumiwa na ukiukaji wa sheria dhidi ya kupata pasi za visa za marekani mbali na kuzuia mali wanazomiliki nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.