Taleban walenga mshirika wa rais Karzai

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 09:19 GMT

Mkuu wa kitengo cha ujasusi nchini Afghanistan Asadullah Khalid, amejeruhiwa katika shambulio la bomu lililokuwa limebebwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, aliyejidai kuwa ni balozi wa amani.

Bwana Khalid alikutana na mshambuliaji huyo nyumbani kwake mjini Kabul ili kujadiliane kuhusu mapatano kati ya kundi la Taliban na serikali.

Kundi la Taliban linasema lilimlenga Khalid, kwa kuwa ni mshirika wa karibu wa Rais Hamid Karzai.

BBC imeambiwa kuwa Khalid amekuwa akitumia zaidi ya nyumba ishirini mjini Kabul kuzuia uwezekano wa shambulio lolote.

Mwandishi wa BBC anasema kumtumia mshambulizi wa kujitoa mhanga anayejidai kuwa mjumbe wa amani, ni mbinu inayotumiwa sana na Taliban.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.