Namna nzige mmoja anavyosababisha baa

Makundi makubwa ya nzige yanazua taharuki Pembe ya Afrika na Asia kusini, wakila mazao na kutishia uhaba wa chakula. Ni uvamizi mkubwa zaidi kwa robo karne iliyopita. Ilikuwaje hali ikawa mbaya hivi?

Picha ya nzige wa jangwani

Nzige wa jangwani kama huyu - aina ya panzi - kawaida hupenda kuishi maisha ya aibu, ya kibinafsi. Anakuwa kutoka yai, kisha nzige mchanga -ajulikanaye kama hopper - na kisha kupevuka mpaka nzige anayeruka.

Picha ya nzige wa jangwani katika hatua ya kundi

Lakini mara kwa mara, hupitia ngazi tafauti za mabadiliko, mathalani wakifika eneo la ukijani wanaacha kuishi kwa kujitenga na kuwa kundi la wadudu hatari.

Katika ngazi hii ya kundi, nzige hubadilika rangi na kuwa katika makundi makubwa yanayopaa kwenda safari za mbali.

Makundi hayo yanaweza kuwa makubwa sana. Kundi linaweza mpaka kuwa na nzige bilioni 10 na kutanda kwenye eneo la mamia ya kilomita. Wanaweza kusafiri kilomita 200 kwa siku moja, huku wakitia hofu na woga maisha ya wakaazi wa vijijini kwa kula mazao yao.

Hata kundi la kawaida tu la nzige linaweza kumaliza mazao ya kuwatosha watu 2,500 kwa mwaka, kwa mujibu wa Sirika la Chakula na Kilimo (FAO), chini ya Umoja wa Mataifa (UN).

Baa kubwa la mwisho la nzige kwa Afrika Magharibi lilikuwa 2003-05 na liligharimu mazao ya thamani ya dola bilioni 2.5 kwa mujibu wa UN.

Lakini kulikuwa na makundi ya nzige pia katika miaka ya 1930, 40 na 50. Baadhi yao walitapakaa katika maeneo mbalimbali mpaka kufikia hatua ya kutangazwa kuwa "baa".

Kwa ujumla, FAO inakadiria kuwa nzige huathiri maisha ya mtu mmoja katika kila watu 10 duniani, jambo linalowafanya kuwa wadudu hatari zaidi wanaohama.

Nzige wa jangwani kama huyu - aina ya panzi - kawaida hupenda kuishi maisha ya aibu, ya kibinafsi. Anakuwa kutoka yai, kisha nzige mchanga -ajulikanaye kama hopper - na kisha kupevuka mpaka nzige anayeruka.

Lakini mara kwa mara, hupitia ngazi tafauti za mabadiliko, mathalani wakifika eneo la ukijani wanaacha kuishi kwa kujitenga na kuwa kundi la wadudu hatari.

Katika ngazi hii ya kundi, nzige hubadilika rangi na kuwa katika makundi makubwa yanayopaa kwenda safari za mbali.

Makundi hayo yanaweza kuwa makubwa sana. Kundi linaweza mpaka kuwa na nzige bilioni 10 na kutanda kwenye eneo la mamia ya kilomita. Wanaweza kusafiri kilomita 200 kwa siku moja, huku wakitia hofu na woga maisha ya wakaazi wa vijijini kwa kula mazao yao.

Hata kundi la kawaida tu la nzige linaweza kumaliza mazao ya kuwatosha watu 2,500 kwa mwaka, kwa mujibu wa Sirika la Chakula na Kilimo (FAO), chini ya Umoja wa Mataifa (UN).

Baa kubwa la mwisho la nzige kwa Afrika Magharibi lilikuwa 2003-05 na liligharimu mazao ya thamani ya dola bilioni 2.5 kwa mujibu wa UN.

Lakini kulikuwa na makundi ya nzige pia katika miaka ya 1930, 40 na 50. Baadhi yao walitapakaa katika maeneo mbalimbali mpaka kufikia hatua ya kutangazwa kuwa "baa".

Kwa ujumla, FAO inakadiria kuwa nzige huathiri maisha ya mtu mmoja katika kila watu 10 duniani, jambo linalowafanya kuwa wadudu hatari zaidi wanaohama.

Nchi ambazo zimeripoti kuvamiwa na nzige 1926-2019
Mwaka Kupungua Kuongezeka ama kwisha Baa
20190180
2018000
2017000
2016500
2015200
2014700
20131000
2012900
2011700
2010400
2009500
2008800
20071300
2006100
20050200
20040230
2003500
2002000
2001000
2000200
1999400
1998700
19971200
19961500
19951500
19941300
19932000
1992500
1991000
1990300
19890150
19880026
19871500
19861200
1985200
1984000
1983700
1982500
1981500
1980600
1979040
19780150
1977300
1976900
1975700
19741100
1973700
1972500
1971400
1970700
19690110
19680250
1967700
1966200
1965400
1964600
19630100
19620290
19610290
19600044
19590047
19580041
19570037
19560035
19550043
19540040
19530043
19520027
19510410
19500330
1949900
19481200
19470290
19460360
19450042
19440047
19430043
19420035
19410240
1940060
1939500
1938300
1937600
1936600
1935600
1934090
19330180
19320027
19310035
19300045
19290041
19280034
19270220
1926080
Chanzo: FAO
Muhimu: Kupungua, inamaanisha kuwa nzige wangalipo japo kwa idadi ndogo; kuongezeka inamaanisha mlipuko wa nzige unaoongezeka kwa kuzaliana; baa inamaanisha mtawanyiko mkubwa na wa nguvu kwa zaidi ya mwaka mmoja; mwisho wa wa baa ndiyo kwisha .

Makundi ya nzige yanahatarisha mazao Afrika Mashariki na Pakistani

Makundi mabaya zaidi ya nzige kwa miongo kadhaa kwa sasa yanavamia mazao kwenye eneo lote la Pembe ya Afrika - kuanzia Djibouti, Eritrea, Ethiopia na Somalia - na kwengineko, na kutishia baa la njaa katika eneo lote hilo.

Nzige hao kwa sasa wanasambaa nchini Kenya baada ya kuzua balaa Somalia na Ethiopia. Ni mlipuko mkubwa zaidi kwa Kenya kwa zaidi ya miaka 70, huku Somalia na Ethiopia miaka 25.

Somalia imetangaza janga la kitaifa. Ni nchi ya pili kufanya hivyo baada ya Pakistani ambapo wameharibu mazao ya pamba, ngano, mahindi na mazao mengine.

Lakini ni eneo la Pembe ya Afrika, wanasema FAO, ambapo mazalia ya nzige yamekuwa mara 500 zaidi kufikia Juni.

Nchi ambazo zipo kwenye hatari ya kuvamiwa na nzige

Ramani inayoonesha makundi ya nzige Pembe ya Afrika, Bahari ya Shamu na mpaka wa Indai na Pakistani. Nzige pia wapo Kenya na Ethiopia na wanaweza kuingia nchi nyengine. Chanzo: FAO, Februari 2020

Baadhi ya makundi ya nzige yamevuka na kuingia Uganda Jumapili, mamlaka za nchi hiyo zimethibitisha na FAO wameonya kuwa linaweza kuwa baa la kanda kama hawatashughulikiwa.

Nzige hao tayari wameshaharibu zaidi ya ekari 175,000 za mashamba Somalia na Ethiopia mwishoni mwa Disemba.

Wanakula tani 1.8 za uoto kwa siku kwa kilomita za za mraba, kwa mujibu wa FAO.

FAO wanaamini kuwa kundi moja la nzige nchini Kenya limesambaa kwenye eneo la kilomita 40 kwa 60.

Je nzige wanaweza kula kwa kiasi gani?

Nzige mkubwa anaweza kula gramu 2 kwa siku. Mchoro unaoonesha kiasi ambacho nzige anaweza kula. Anakula takribani gramu 2 - sawa na uzito wa mwili wake. Kundi la kilomita mraba wanaweza kula sawa na watu 35,000. Chanzo: FAO

Mamlaka za kanda zina hofu kuwa uvamizi wa nzige unaweza kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mazao, na kuhatarisha zaidi upatikanaji wa chakula katika eneo ambalo tayari limeshaathirika na mafuriko na ukame. Zaidi ya watu milioni 20 katika kanda hiyo wanaweza kuathirika, UN inaonya.

"Tunawasiwasi zaidi kwa Kenya na Ethiopia kwa kuwa kuna maeneo mawili ambayo yana makundi mawili makubwa," anasema Keith Cressman, mtabiri mwandamizi wa nzige wa FAO.

"Zaidi, nchini Ethiopia, kuna uzao unaoendelea hivyo nzige wanaongezeka."

Picha ya Ali Bila Waqo, ambaye mazao yake yameharibiwa na nzige.

Ali Bila Waqo, 68, ni mkulima kutoka kaskazini mashariki ya Kenya, alikuwa akitegemea mazao mazuri msimu huu, baada ya mvua za hivi karibuni baada ya ukame.

Lakini nzige wameteketeza mahindi na maharage yake yote.

"Wamekula mazao yetu karibu yote, na ambayo hawakula yalinyauka," anasema. "Hii imetuumiza sana. Tumekiona chakula kwa macho yetu, lakini hatukuweza kukifurahia."

Bwana Waqo, ambaye anakumbuka uvamizi mwengine miaka ya 1960, aeleza namna gani nzige hao walivyofanya anga kuwa la giza.

"Kulikuwa kweusi na usingeweza kuliona jua," amesema.

Hali mbaya ya hali ya hewa imesababisha janga hili.

Chanzo cha uvamizi huu kinaanzia kwenye vimbunga na mvua kubwa kwa 2018-19.

Nzige wa jangwani kwa kawaida huishi katika maeneo makavu baina ya nchi 30 kuanzia Afrika Magharibi mpaka India - eneo ambalo lina kilomita za mraba milioni 16.

Hata hivyo, unyevu na hali ya hewa nzuri kwao kwa miaka miwili chini ya Rasi ya Uarabuni ikaruhusu vizazi vitatu vya nzige kutanuka bila kubainika, UN inaeleza.

Nzige hao wamekuwa wakizaliana toka 2018.

Ramani inayoonesha jinsi gani nzige walivyokuwa wakizaliana kwa misimu kadhaa na kuhama kutoka Arabuni mpaka Pembe ya Afrika na mpaka wa India na Pakistani. Chanzo: FAO, Januari 2020.

Kufikia mwanzoni mwa 2019, makundi ya mwanzo yalihamia Yemen, Saudi Arabia na Iran na kuzaliana zaidi kabla ya kuhamia Afrika Mashariki.

Makundi zaidi yalijitengeneza na kufikia mwishoni mwa 2019 yakaongezeka Eritrea, Djibouti na Kenya .

Picha za makundi ya nzige katika eneo la Samburu, Kenya.

Makundi hayo pia yanakuwa katika pande zote mbili za Bahari ya Shamu na kuathiri nchi za Misri, Sudani, Saudi Arabia na Yemen, pamoja na mpaka wa India na Pakistani - hali ambayo UN imeieleza kuwa ni "hatarishi sana".

Japo uvamizi huo ni mgumu kupambana nao kutokana na eneo kubwa ambalo nzige hao huathiri, Bw Cressman wa FAO anaamini kuwa udhibiti wa awali ungeweza kufanyika.

"Kama kungekuwa na hatua kubwa na za ufanisi za udhibiti katika nchi muhimu, ingeliwezekana kupunguza ukubwa wa hali ya sasa," amesema.

Watu wakijaribu kupambana na makundi makubwa ya nzige

Kwa kuwa makundi ya nzige yapo Pembe ya Afrika tena kwa ukubwa usiomithilika na uwezo mkubwa wa uharibifu, nchi jirani zinahangaika kupambana nao.

Kuwazuia kunategemea mambo makuu mawili - uangalizi na njia sahihi za udhibiti .

Kituo cha Taarifa cha Nzige wa Jangani, ambacho kinaendeshwa na FAO, kinatoa taarifa za utabiri, onyo la awali, muda, ukubwa na eneo la uvamizi na kuzaliana.

Lakini idadi ya nzige inapofikia kiwango hatarishi, kama hali ilivyo kwa Pembe ya Afrika, hatua za haraka hutakiwa kuchukuliwa ili kupunguza idadi, pamoja na kuzuia makundi kujikusanya na kusambaa.

Jinsi gani makundi ya nzige hudhibitiwa

Mchoro unaonesha namna gani nzige wanaweza kudhibitiwa kupitia unyunyuziaji wa dawa kupitia kutembea kwa miguu, kwa ndege ama magari. Chanzo: FAO

"Operesheni kubwa ya anga inahitajika kwa saasa nchini Kenya na Ethiopia - na pia Somalia japo hilo haliwezekani kutokana na hali ya kiusalama," anasema Cressman.

"Kwa kuwa washakuwa wakubwa, itakuwa vyema zaidi kuwashambulia [nzige] kwa kutumia ndege ili kupunguza idadi ya wale watakaopevuka na na kutaga mayai."

Japo kwa sasa hakuna utafiti juu ya suluhisho bora zaidi la kimazingira, kama dawa za kibailojia ama wadudu wanaoshambulia nzige, njia ya kawaida zaidi ya udhibiti inayotumika ni unyunyuziaji wa dawa.

Kuwanyunyizia nzige kupitia pampu za mkono, magari au ndege, makundi hayo yanaweza kuteketezwa kwa kemikali kwa muda mfupi.

Juhudi za kupambana na uvamizi wa nzige nchini Kenya zimeongezeka kwa kutumia unyunyuziaji wa ndege, lakini kukabiliana na makundi makubwa katika eneo kubwa na la mbali bado ni changamoto kubwa.

Picha ya mazao yaliyoharibiwa ya mkulima Ali Bila Waqo

Ni jambo gumu zaidi kwa nchi ambazo hazijapambana na nzige kwa muda mrefu kwa kuwa hakuna miundombinu na kumbukumbu ya mapambano.

"Inaweza kuzusha taharuki kubwa pale nzige wanaporejea," anasema Cressman.

Hatua zilizochukuliwa Somalia, Ethiopia na Kenya - pamoja na Pakistan- ndizo zitakazoamua nini kitakachotokea. Kama nzige wataendelea kuvuka mipaka zaidi na kuathiri maeneo mengine, na kuharibu mazao zaidi basi uvamizi huo utatangazwa kuwa "baa".

UN inaeleza kuwa operesheni za angani na ardhini kwa sasa hazitoshelezi na kuiomba jumuiya ya kimataifa kutoa dola milioni 70 kama msaada wa dharura kukabiliana na nzige hao.

Lakini kwa mkulima wa Kenya Ali Bila Waqo na familia yake, hatua yoyote kwa sasa itakuwa imeshachelewa. Kitu pekee ambacho waliweza kufanya kudhibiti nzige walipovamia ni kupiga madebe na kelele.

Hata hivyo, bado anakitazama kilichotokea kwa jicho la falsafa.

"Ni mapenzi ya Mungu. Hili ni jeshi lake," anasema.

Utambuzi

Maneno na uzalishaji na Lucy Rodgers, uzalishaji na Joe Inwood, usanifu na Zoe Bartholomew na Millie Wachira, uendelezaji na Becky Rush, Catriona Morrison na Purity Birir. Picha za nzige na Swidbert R Ott na Stephen Rogers na Getty Images. Picha za wakulima Kenya na BBC.


Maelezo zaidi kuhusu habari hii