Usaidizi na Maswali yaulizwayo mara kwa mara

Jinsi ya kutumia vyema tovuti hii

Jinsi ya kuangalia video na kusikiliza sauti katika tovuti

Milisho ya RSS – ni kitu gani?

Editorial FAQ

GMT ni nini?

Jinsi gani naweza kusikiliza Bbcswahili kwa njia ya radio?

Ninawezaje kuboresha upokeaji wangu wa matangazo?

Kusikiliza redio katika Masafa Mafupi

Fomu ya mwitikio / Hoja ambazo hazijapatiwa ufumbuzi

Jinsi ya kutumia vyema tovuti hii

Tovuti hii imejengwa kwa ajili ya skrini yenye msongo wa upana wa piseli 1024. Endapo unatumia skrini yenye msongo mdogo, unaweza kubiringisha kwa mlalo ukaweza kufikia maudhui yote. Njia mbadala inaweza kutumia toleo la tovuti lenye picha kidogo. Baadhi ya vipengee vya tovuti vinaweza tu kufanya kazi endapo Javascript imewezeshwa katika kivinjari chako.

Kuwezesha Javascript: Internet Explorer kwa ajili ya Windows: Nenda kwenye Tools menu katika IE na chagua Internet Options; bofya Security tab; Hakikisha kuwa Internet Zone imeangazwa kisha bofya kitufe cha Custom Level kufungua chaguo za usalama; Angalia sehemu iliyoandikwa Scripting, kisha Active Scripting na hakikisha kuwa imewezeshwa; Bofya OK kufunga paneli; Sasa pakia upya ukurasa unaohitaji Javascript.

Internet Explorer kwa ajili ya Mac: Tafuta Preferences kwenye menyu ya Explorer. Chagua orodha ya Web Content kutoka upande wa kushoto wa dirisha; Tafuta kipengele cha Active Content. Hakikisha kuwa kisanduku kando na Enable Scripting kimeteuliwa; Bofya kitufe cha OK. Funga dirisha dirisha na bofya kitufe cha Refresh cha ukurasa unaohitaji Javascript; Kuwezesha Java, bofya kiunganishi cha Java kwenye kifungu cha Web Content.

Safari: Nenda kwenye menyu na chagua Preferences; bofya Security tabo; Unaweza kuteua au batilisha uteuzi wa vyote Java na Javascript hapa.

Firefox: Nenda katika menyu ya Tools na teua Options; kisha bofya Web Features. Teua Enable Javascript (au Java) katika paneli kuu na bofya OK.

Opera: Kwenye menyu ya Tools, bofya Quick Preferences; bofya Enable JavaScript.

Jinsi ya kuangalia video na kusikiliza sauti katika tovuti

Video na sauti katika Bbcswahili.com zinaweza kupatikana katika maeneo tofauti ya tovuti, kama viunganishi vinavyojitegemea au zikiwa zimefutikwa ndani ya habari zinazohusiana. Ili kuweza kucheza kipogo, unaweza kuhitaji kuunganisha wavuti yenye kasi isiyopungua 56kbps, lakini utapata matokeo mazuri zaidi kwa kutumia wavuti yenye kasi – broadband connection.

Kwa vipogo vilivyofutikwa katika habari, utahitaji programu-jalizi ya Flash Player kwa kivinjari chako.

Bofya hapa kupakua Flash Player*:

Kupakua Flash Player

Kwa mafaili mengine ya sauti na video, utahitaji kati ya Real Player au Windows Media Player.

Bofya kupakua Real Player*:

Kupakua Real Player

Bofya kupakua Windows Media Player*:

Kupakua Windows Media Player

* Kanusho la upakuaji: Programu-jalizi zote unazohitaji kutumia maudhui yote katika bbc.co.uk ni BURE kupakua na kutumia. Kamwe hauhitaji kulipa chochote au kutoa maelezo ya kadi yako ya benki. Wakati unapakua programu-jalizi hizi, utatakiwa kukubaliana na kanuni na masharti ya makampuni husika. Hii haihusishi BBC. Pia watatakiwa kukueleza watafanya hivyo kwa kutumia maelezo yako.

Milisho ya RSS + ATOM

Milisho ya RSS inakuwezesha kuona wakati tovuti inapoongeza maudhui mapya. Unaweza kupata vichwa vya habari mpya na video katika eneo moja, kadri zinavyochapishwa, bila kuzuru tovuti ambazo umejiunga kwa mlisho.

Kumekuwa na mijadala kujiuliza RSS maana yake nini, lakini watu wengi huita 'Really Simple Syndication'. Kwa kifupi, milisho yenyewe ni kurasa za tovuti, zilizosanifiwa kusomwa na kompyuta badala ya watu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu milisho ya RSS na jinsi ya kuitumia bofya hapa:

Milisho ya RSS ni nini?

Editorial FAQ

Maswali ya kihariri yanayoulizwa mara kwa mara

GMT ni nini?

Greenwich Mean Time (GMT) ni muda unaopimwa katika nyuzi sifuri kwenye mstari wa longitudi au meridian. Huu unapita kutoka Ncha ya Kaskazini mpaka Ncha ya Kusini, kupitia kitongoji cha Greenwich mjini London ilipo Old Royal Observatory.

Mstari huu ulianza kuitwa Greenwich Meridian tangu mwaka 1884, na kuanzia wakati huo muda wa dunia umekuwa ukipimwa na kuhesabiwa kwa utaratibu huo.

Kwa ujumla, endapo upo katika nchi iliyo mashariki mwa Greenwich Meridian, muda wa mahali ulipo utakuwa mbele ya GMT (mfano muda nchini China ni saa nane mbele ya GMT - GMT +8 hours).

Magharibi mwa Greenwich Meridian, muda unakuwa nyuma ya GMT ( mfano muda mjini New York ni saa tano nyuma ya GMT kipindi cha majira ya baridi na wakati wa majira ya joto ni saa nne).

Jinsi gani naweza kusikiliza Bbcswahili kwa njia ya radio?

Katika kuongezeka kwa idadi ya maeneo, inawezekana kusikia vipindi vya BBC World Service kupitia masafa ya FM au AM katika eneo lako (tembelea ukurasa wetu wa masafa au frequency kwa maelezo). Hata hivyo katika maeneo mengi tunaendelea kutangaza kupitia masafa mafupi ya radio.

Masafa mafupi ya radio

Ili kusikiliza BBC World Service katika masafa mafupi, radio yako ni lazima iwe inapopkea sehemu kubwa ya mita bandi zilizoorodheshwa hapa chini. on short wave, your radio receiver must cover most of the broadcast bands listed below. If you have a receiver with a dial, these bands may be shown either as frequencies or as wavelengths. A radio with an electronic display shows frequencies.

Maelezo ya masafa ya BBC World Service kwa kawaida yanatolewa katika kilohertz (kHz) ispokuwa pale imeelezwa vinginevyo. BBC World Service inatangaza kupitia mita bendi zifuatazo (m). Mfano wa masafa katika kila bendi yanaonyeshwa katika kilohertz (kHz) na Megahertz (MHz):

Ninawezaje kuboresha upokeaji wangu wa matangazo?

Vipimo vya masafa mafupi/Short-wave vinasafiri kutoka kwenye transmita hadi kwenye radio yako kwa kugongwa kati ya ionosphere (leya yenye gasi ya umeme mamia ya kilometa kadhaa juu ya ardhi) na uso wa dunia. signals travel from the transmitter to your radio by being bounced between the ionosphere (layers of electrified gas several hundred kilometres above the earth) and the earth's surface.

Gasi katika ionosphere mara kwa mara zinaweza kusababisha upokeaji wa matangazo kutofautiana katika kiwango kati ya mchana na usiku, msimu wa kiangazi na baridi na hata wakati kipindi cha saa chache. Vipimo vinaweza kuathiriwa na dhoruba kali,maeneo ya milima na, katika miji yenye majengo marefu.

Njia ya kuweza kupokea matangazo vizuri zaidi

Iwapo radio yako inatumia bateri, huna budi kuhakikisha kuwa batteri ni nzima na zina nguvu, la sivyo upokeaji wa matangazo utakuwa mgumu iwapo batteri ni dhaifu. Spika za radio ndogo mara nyingi ni ndogo, lakini ubora wa sauti mara nyingine unaweza kuboreshwa kwa kutumia spika ndogo za masikioni (headphones) au spika kubwa za nje ya radio. Jaribu kuweka radio katika muelekeo tofauti: matangazo hupokelewa vizuri kupitia dirishani, hususani upande unaongalia muelekeo wa transmita. Katika kila eneo la masafa yetu mafupi kuna alama inayoonyesha eneo ilipo transimita kwa kila frequency. Ingawaje kuweka radio juu ya kifaa cha chuma kunaweza kusaidia, sehemu kubwa ya ujenzi wa chuma kama vile milango ya dharura, lifti, n.k vinaweza kusababisha mwingiliano. Hali kadhalika vifaa vya umeme majumbani kama vile kompyuta na mashine za kupashia chakula joto au microwave ovens.

Antenna yako (aerial)

Huna budi kujaribu kwa pamoja urefu na uelekeo wa antenna ya radio yako. Huenda ukakabiliana na mapokezi hafifu ya matangazo iwapo unajaribu kusikiliza ndani jingo lililojengwa kwa vyuma, lakini iwapo mapokezi yanaboreka wakati ukichukua radio yako karibu na dirisha, antenna ya nje inaweza kusaidia. Mara kwa mara kitu muhimu ni kufunga kipande cha waya wa shaba kutoka umbali wa mita chache kuzunguka mahali antenna ya radio yako ilipo. Ning’iniza upande wa mwisho wa waya nje ya dirisha, ukiweka mbali kabisa na vifaa vya chuma au nyaya za umeme. Radio nyingi ndogo zenye ubora wa masafa mafupi zimebuniwa kutumika pasipo kutumia antenna ya nje, kuongezea antenna ya ziada wakati mwingine kunaweza kusababisha radio kuelemewa, kwa hiyo haishauriwi kuongezea antenna ya ziada pasipo kufanya majaribio kwanza.

Onyo

Ni muhimu kukumbuka kwamba antenna yoyote ya nje ambayo ina nguvu kubwa ya umeme inaweza kutengeneza radi. Wakati wa dhoruba, huna budi kukata kiunganishi cha antenna ndani ya nyumba au tupa nje kupitia dirishani.

Ni jinsi gani ya kutengeneza antenna rahisi ya ziada kwa kupokea masafa mafupi Iwapo unataka kutengeneza antenna ya ziada ya kudumu kwa radio yako, hii inaweza kufanyika kwa kutumia waya wenye urefu wa kama mita 10 hivi. Upande mmoja unapaswa kuunganishwa kwenye tundu la antenna ya radio. Baadhi ya radio zinatumia kifaa kinachoitwa jack connector plug cha ukubwa wa 3.5 mm, kinachotakiwa kuchomekwa katikati au katika ncha na kuacha sehemu ya nje wazi.

Sehemu kubwa ya waya kadri inavyowezekana inapaswa kuachwa nje ya jengo, kwa kulazwa chini au katika nyuzi kama 30 hivi kutoka ardhini, kati ya dirisha na kishikizo (mfano mti). Iwapo hii haiwezekani basi ning’iniza juu ya dirisha mbali na vifaa vya chuma na nyaya za umeme.

Uwiano wa waya ndani ya jengo unaweza kuchukua mwingiliano wa vifaa vya umeme majumbani, lakini hii inaweza kuepukika kwa kutumia kifaa kinaitwa kinaitwa coaxial au "screened" cable kwa sehemu hii ya ncha ya antenna. Kwa ajili hii, For this, the centre core of the coaxial cable should be connected to the aerial wire, with the outer braiding of the cable left unconnected

Kwa upande wa radio, kisha sehemu kuu ya katikati ya waya inapaswa kuunganishwa katika tundu na At the radio end, the centre core of the cable should then be connected to the plug at the tip contact and the outer braiding to the sleeve. However, it is not a good idea to use more than a couple of metres of coaxial cable, as long lengths can affect the signal.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii